Arteta: kuhusu Ubingwa bado sana
Sisti Herman
February 8, 2026
Share :

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amedai uongozi wa pointi tisa kileleni mwa Ligi Kuu England “haumaanishi chochote” licha ya timu yake kuongeza shinikizo kwa Manchester City iliyopo nafasi ya pili.
Washikabunduki hao walishinda mabao 3-0 dhidi ya Sunderland Jumamosi, huku Martín Zubimendi akianza kufunga bao dakika ya 42, kabla ya Viktor Gyökeres kufunga mara mbili.
Wao Man City wana nafasi ya kupunguza pengo la pointi kama leo Jumapili wataifunga Liverpool.
Lakini alipoulizwa na waandishi wa habari baada ya mchezo huo kuwa pengo hilo linamaanisha nini katika hatua hii ya msimu, Arteta alijibu:
"Hakuna. Bado tunapaswa kushinda michezo mingi ili kufikia kile tunachotaka, kwa hiyo lazima tuzingatie hilo, ni jambo lingine, tumefanya kazi yetu sasa, tumepata tunachopaswa kufanya, tanathmini hilo, tunajaribu kujiboresha na kujiandaa kwa mchezo wetu dhidi ya Brentford Alhamisi."





