pmbet

Arteta usipopata kombe utatujibu ni kwanini - Henry

Eric Buyanza

May 2, 2026
Share :

Gwiji wa Arsenal, Thierry Henry, amemwambia kocha Mikel Arteta kwamba atalazimika kujibu maswali magumu kutoka kwa bodi ya klabu ikiwa atashindwa kushinda kombe lolote msimu huu.

 

Kikosi cha Arteta kwa sasa kinashindana kushinda Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu. Wamekaa kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu wakiwa na pointi tatu mbele ya Manchester City walio katika nafasi ya pili, ambao wana mchezo mkononi.

 

Arsenal pia itamenyana na Atletico katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumanne kuwania kufuzu fainali. Akiongea na CBS Sports, Henry alisema, "Bodi italazimika kuamua watafanya nini na Mikel Arteta. Ninachosema ni kwamba baada ya miaka yote hiyo na kiasi cha pesa kilichotumika tumekuja kukubaliana kuwa Arsenal wana kikosi bora zaidi msimu huu....Itabidi uzungumze na kujibu maswali kadhaa ikiwa hautashinda kombe.”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet