pmbet

Arudiana tena na mwanamke aliyemkata uume wake!

Eric Buyanza

April 10, 2024
Share :

Mwanamume mmoja huko nchini Brazil amemrudia mpenzi wake wa zamani ambaye alikata uume wake siku alipogundua ana uhusiano wa kimapenzi na binti wa miaka 15.

Gilberto Nogueira alikuwa akiishi vizuri na mpenzi wake Daiane dos Santos, mpaka siku ile alipogundulika alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpwa wa Daiane mwenye umri wa miaka 15.

Baada ya kugundua jambo hilo, Daiane hakuongea lolote bali aliamua kulipiza kisasi kimyakimya bila kumwambia yeyote.


NINI KILITOKEA?

Usiku mmoja mwezi December mwaka jana 2023, jamaa akiwa amelala kitandani bila nguo, Daiane aliingia chumbani na kuzima taa kisha akaufunga uume wa Gilberto kwa mpira na kuanza kuukata kwa wembe.

Baada ya kuukata aliupiga picha na kuwarushia ndugu wa Gilberto kwenye magroup ya whatsApp na kisha akautupa chooni.

Tangu wakati huo Gilberto amefanyiwa upasuaji mara nyingi kutokana na jeraha alilopata na hivi sasa anasubiria kuwekewa uume wa bandia.

Katika mahojiano aliyofanyiwa mwezi Februari, Gilberto alisema mwanamke huyo anastahili kukaa jela kwa kuwa ni ‘mhalifu.’

Kwasasa mwanamke huyo yuko kizuizini akisubri kuanza kwa kesi yake April 24.

Hata hivyo Gilberto amewashangaza wengi baada ya kufanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini humo, msikilize; 

"Kama sikufanya mapenzi na mpwa wake haya yasingetokea" Gilberto alikiambia chombo hicho cha habari" anaendelea....."Daiane ni mwanamke mzuri na mwenye upendo ambaye ananipenda. hakustahili kusalitiwa kama nilivyofanya" akasema Gilberto.

Mwanamke huyo amekuwa akiwasiliana kwa barua na Gilberto na tayari wameshasameheana kwa yaliyotokea.

Na haya ni baadhi ya maneno aliyoyaandika Giberto kwenye barua iliyofumwa akimuandikia mwanamke huyo aliyemtia kilema cha maisha......

"Leo, nitakuambia kile kinachoendelea moyoni mwangu. Nataka utoke huko haraka iwezekanavyo ili uje unitunze.....Nahesabu siku za wewe kurudi nyumbani. Siku ambayo utaachiwa huru, ujue kwamba nitakuwa nje ya mlango wa gereza kukusubiri kwa mikono miwili.’ alimalizia Gilberto.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet