pmbet

Asake amzawadia mama yake G-Wagon ya Mabilioni ya fedha.

Joyce Shedrack

March 3, 2026
Share :

Staa wa Muziki wa Afrobeats Asake amemzawadia mama yake gari Jipya G-Wagon 63 nyeupe ikiwa ni katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
 

Katika video ya kugusa moyo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwimbaji wa wimbo wa "Lonely At The Top" alionekana akimkabidhi gari la kifahari mama yake katika tukio lililoonekana kuwa la faragha lakini lenye hisia kubwa.

 

Gari la Mercedes-Benz G-Wagon la rangi nyeupe, ambalo inaripotiwa kuwa na thamani ya mamia ya milioni za naira, lilifungwa vizuri na likakabidhiwa kama zawadi maalum ya Ramadhan.

 

Mashabiki zake kutoka katika mitandao ya kijamii wameonekana kufurahishwa na jambo hilo wakimsifu mwimbaji huyo kwa kumheshimu mama yake kwa njia ya kifahari kama hiyo.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet