“Asanteni kwa kuniombea, wengine walisema Mzee amakata moto” - Dk Mpango
Eric Buyanza
December 10, 2023
Share :
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amerejea nchini alfajiri ya leo tarehe 10 Desemba 2023 na moja kwa moja alihudhuria ibada ya Jumapili leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska .
Akiongea na waumini baada ya ibada hiyo amewaasa watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii kwani matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi.
Makamu wa Rais amesema kwa takribani mwezi mmoja ambao hakuwa nchini huku mengi yakiongelewa juu yake, alikuwa nje ya nchi kwa ajili ya shughuli maalumu.
“Asanteni sana kwa kuniombea. Yamesemwa mengi si ndio? Na wengine wanasema mimi ni mzuka.......Wengine wanasema mzee amakata moto….lakini bado kabisa, kazi ambayo Mungu amenituma kufanya sijaimaliza.” amemalizia Dk Mpango.