pmbet

Asha aenda jela maisha kwa kumbaka mvulana wa miaka 15

Eric Buyanza

April 4, 2024
Share :

Mahakama Wilaya ya Mtwara, imemhukumu kifungo cha maisha jela, Asha Chanchoni (47) kwa kosa la shambulio la aibu, baada ya kubainika kujihusisha kimapenzi na mvulana mwenye umri wa miaka 15.
 

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Lucas Jang’andu aliyesema Mahakama imethibitisha bila kuacha shaka kuwa mwanamke huyo alikuwa akijihusisha kimapenzi na mvulana huyo.

Kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi wawili wa upande wa Jamhuri, tukio hilo lilitokea Februari 2023 katika mtaa wa Chuno katika manispaa ya Mtwara Mikindani anakoishi mwanamke huyo.
NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet