Asilimia 60 ya majeruhi wa ajali za bodaboda huumia kwenye Ubongo
Eric Buyanza
March 26, 2024
Share :
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Prof Abel Makubi amesema asilimia 60 ya majeruhi wa ajali hasa bodaboda wanaumia sehemu za ubongo.
Prof Makubi ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Kimataifa wa wataalamu wa ubongo,mishipa ya fahamu na uti wa mgongo ulioandaliwa na MOI kwa kushirikiana na chuo na Hospitali ya Well Cornel cha nchini Marekani.
“Kwa wastani kwenye idara ya magonjwa ya dharura tunapokea wagonjwa 15 hadi 20 ambao wanatokana na dharura mbalimbali na asilimia 60 zinatokana na ajali na wengi ni bodaboda, tatizo ni kubwa wengi wanakuwa wameumia mifupa na ubongo,” ameeleza.