pmbet

Asilimia 99.5 ya wagonjwa wa dharura wanaofika Muhimbili wanapona

Eric Buyanza

May 11, 2024
Share :

Asilimia 99.5 ya wagonjwa wote wanaopokelewa katika Idara ya Tiba ya Magonjwa ya Dharura, Hospitali ya Taifa Muhimbili wanauhakika wa kupatiwa huduma za matibabu kwa wakati na afya zao kuimarika.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Dkt. John Rwegasha, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji katika maadhimisho ya miaka 10 ya ushirikianao ulipo baina ya Muhimbili na Mfuko wa Abbott Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma za Tiba ya Magonjwa ya Dharura hospitalini hapo.
 

Dkt. Rwegasha amesema uhusiano huo umesaidia kuboresha huduma za magonjwa ya dharura kwa kiwango kikubwa na kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa hayo ambapo kwa sasa vifo vimepungua na kufikia chini ya asilimia 0.5.
 

“Zamani ulikuwa ukisikia watu wakilalamika kuwa wagonjwa wa dharura wakifika hapa wanapoteza maisha ila kwa sasa malalamiko hayo hakuna tena kwakuwa huduma zimeboreshwa,”amesema Dkt. Rwegasha.
 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Tiba ya Mgonjwa ya Dharura MNH Dkt.Juma Mfinanga amesema kuwa idara hiyo inatoa huduma zote muhimu ikiwemo huduma ya upasuaji hivyo mgonjwa atakayepokelewa katika idara hiyo anapatiwa huduma zote za awali kabla ya kupelekwa wodini.
 

Pamoja na hayo amesema idara hiyo ndiyo idara ya mfano kwa hospitali zote hapa nchini na kwa kwakuwa hakuna wagonjwa wote wanaofika Muhimbili wakiwa na dharura wanapatiwa huduma kwa wakati.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet