pmbet

Askari auawa na mkewe kwa panga, kisa kuchelewa kurudi nyumbani!

Eric Buyanza

April 5, 2024
Share :

Huko Kiplombe nchini Kenya, Ofisa wa polisi wa kitengo maalum ameuawa kwa kuchomwa na panga na mkewe kisa kikidaiwa ni kuchelewa kurudi nyumbani. 

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Ofisa huyo aliyefahamika kwa jina la Vincent Kipterim alishambuliwa kwa panga na mke wake aliyefahamika kwa jina la ZamZam Bashir (26) baada ya kufika nyumbani mishale ya saa 9 alfajiri, Jumanne ya Aprili 2, 2024. 

Inaelezwa na mashuhuda kuwa baada ya Vincent kufika akiwa amechelewa kulizuka ugomvi mkubwa baina yao, ugomvi ambao ulisababisha Vincent kuchomwa na panga ambapo alikimbizwa Hospitali kwa matibabu lakini alifariki muda mchache baadae kutokana na majeraha.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet