pmbet

Askari wazingira nyumba ya Bobby Wine Uganda

Sisti Herman

January 19, 2024
Share :

Kufuatia  Maandamano yaliyopangwa kufanyika Jijini Kampala, Nchini Uganda Vyombo vya usalama vya nchini humo vimezingira nyumba za Wanasiasa wa upinzani Kizza Besingye na Bobi Wine.

 

Msanii maarufu nchini humo ambaye pia ni mwanasiasa Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi ameandika kupitia mtandao wake wa X kuwa wanajeshi wamezingira nyumba yake.

 

Bobi Wine ameandika  ”Wanajeshi waoga pamoja na Polisi wamezingira nyumba zetu , ili tusitoke hata hivyo maandamano yanaendelea”.

Polisi wameahidi kuzuia maandamano yaliyopangwa kufanyika dhidi ya hali dhaifu ya barabara mjini Kampala.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet