Askofu anusurika kifo madhabahuni
Joyce Shedrack
April 16, 2024
Share :
Askofu Mar Mari Emmanuel wa kanisa la Orthodox ‘Good Shepherd Church jijini Sydney, Australia amenusirika kifo baada ya kuvamiwa wakati akihubiri madhabuhuni na kushambuliwa kwa visu tukio lililotokea Jumatatu saa moja ya jioni.
Ripoti kutoka nchini humo zinasema Askofu yuko salama na majeraha siyo makubwa sana, katika tukio hilo waliojeruhiwa ni watu wawili tu akiwemo Askofu.
Askofu Emmanuel anajulikana kama moja ya Wachungaji wenye misimamo mikali na mkosoaji wa jambo lolote lisilokua sahihi kibiblia, akiwa ni miongoni mwa viongozi wa Dini ya Kikristo wanaopinga waziwazi sera ya mapenzi ya jinsia moja (Ushoga).
Kwa wafuatiliaji wa mafundisho ya mtandaoni huwezi kuwa hujawahi kumwona Askofu huyu kwakua ni moja ya watu wenye umaarufu mkubwa mtandaoni.
Tayari Jeshi la Polisi nchini Australia wanamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 17 kwa tuhuma hizo.