Askofu Mkuu wa Methodist akutwa amejinyonga Dodoma
Sisti Herman
May 17, 2024
Share :
Askofu Mkuu wa makanisa ya Methodist, Joseph Bundala amekutwa amejinyonga kwenye jengo la kanisa lake lililopo kwenye mtaa wa Ipagala uliopo wilaya ya Dodoma mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mwili wa Askofu Bundala ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Makanisa ya Methodist Afrika uligundulika saa 3 usiku jana, Mei 16, 2024.