Aslay sio wa mchezo mchezo - Mboso
Eric Buyanza
December 16, 2023
Share :
Msanii kutoka WCB 'Mbosso', amesema ikitokea msanii mwenzake Aslay akajiunga na lebo hiyo...ataongeza kitu kikubwa kwa kuwa ni msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuimba na pia atasaidia kuimarisha zaidi lebo ya kundi hilo.
“Mi napenda sana wasanii wenzangu wafaidike na vipaji vyao hivyo endapo Aslay atajiunga na WCB itaongeza kitu, Aslay sio wa mchezo ni msanii mkubwa na mwenye uwezo wa kuimba,” anasema Mboso ambaye hapo zamani yeye na Aslay walikuwa kati ya wasanii waliokuwa wakiunda kundi la "Mkubwa na Wanawe' lililokuwa likisimamiwa na Mkubwa Fella.