pmbet

Atakayeweza kumzuia Ufaransa kubeba ndoo ni Argentina pekee - Ian Wright

Eric Buyanza

July 2, 2026
Share :

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Ian Wright, ameitaja timu pekee inayoweza kuizuia Ufaransa kuchukua Kombe la Dunia, na timu hiyo ni Argentina.

 

Mkali huyo wa soka amefafanua kuwa Ufaransa kwa sasa wanaonekana kutozuilika kutokana na safu yao hatari ya ushambuliaji inayoongozwa na Kylian Mbappé. Hata hivyo, anaamini Argentina inaweza kuwazuia kwa sababu tabia yao ya kuwa wapiganaji uwanjani.
 

“Ili kuwazuia mastaa wa Ufaransa kama Mbappé na Ousmane Dembélé, ni lazima kuwachezea mchezo mgumu na wa kuwapa presha kubwa jambo ambalo Argentina wanalimudu vyema.”
 

"Itahitajika juhudi kubwa kuifunga Ufaransa.......Itahitajika timu kama Argentina kutokana na roho ya kivita waliyonayo." alisema Wright.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet