Atapeliwa milioni 129 na Elon Musk wa bandia
Eric Buyanza
May 4, 2024
Share :
"Julai 17 mwaka jana 2023, Elon Musk alini-follow Instagram. Ingawa nimekuwa shabiki wake mkubwa lakini nilitilia shaka kidogo," alisema mwanamke mmoja wa Korea Kusini aliyekataa kutaja jina lake wakati akihojiwa na kipindi cha "In Depth 60 Minutes".
Mwanamke huyo anasema alianza kuamini kuwa anaongea na Bilionea halisi baada ya mtu huyo kumtumia picha za kitambulisho chake na pia kumtumia picha zake akiwa kazini na kuna wakati waliweza kuzungumza kupitia video (video call).
Baada ya kuona ameshaaminiwa, tapeli huyo (Elon Musk feki) alimshawishi mwanamke huyo kuhamisha pesa kiasi cha $50,000 sawa na (Milioni 129 za kibongo) kwenda kwenye akaunti aliyosema ni ya mfanyakazi wake wa Korea na kumwambia anajisikia furaha akiona mashabiki zake wakitajirika huku akimuahidi kumtajirisha kutokana na hela hiyo aliyoitoa kama uwekezaji kwenye kampuni yake.
Hata hivyo baadae ilikuja kugundulika mwanammhe huyo alikuwa tayari ameshaingia kwenye mfumo wa tapeli kwa njia ya Akili Bandia (Artficial Intelligence).