Atembea 800 km kumpelekea Rais kuku wa kienyeji
Sisti Herman
September 7, 2026
Share :

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesherehekea ushindi wake na wafuasi wake wawili: mmoja kati yao ni yule aliyetembea zaidi ya kilomita 800 na kumpa zawadi ya "kuku wa kienyeji" katika mji mkuu Lusaka, na mwingine aliendesha baiskeli kwa takriban kilomita 470 kuhudhuria kuapishwa kwake kufuatia ushindi wake katika Uchguzi Mkuu.
Rais wa Zambia, ambaye awali aliingia madarakani mwaka 2021, aliapishwa kwa muhula wa pili tarehe Septemba 1, baada ya kushinda uchaguzi wa mwezi uliopita, kwa mujibu wa matokeo rasmi ya Tume ya Uchaguzi.





