Atemwa Man City baada ya miaka 6 na kucheza dakika 108.
Joyce Shedrack
June 9, 2025
Share :
Klabu ya Manchester City imeachana na golikipa wake raia wa Uingereza Scott Paul Carson (39) baada ya kuhudumu kwenye kikosi chao kwa miaka sita akifanikiwa kucheza dakika 108 tu na kushinda mataji 11.
Carson anamaliza mkataba wake ndani ya Man City mwishoni mwa mwezi huu hivyo pande zote mbili zimekubaliana kutokuongeza mkataba mpya na mchezaji huyo.
“Tungependa kumshukuru Scott kwa kujituma na kujitolea na tunamtakia kila la kheri na bahati njema kwa ajili yake siku za usoni” imesema sehemu taarifa ya klabu hiyo.