pmbet

Atetico kuwashtaki Barcelona FIFA kisa Julian Alvarez.

Joyce Shedrack

June 23, 2026
Share :

Klabu ya Atletico Madrid imepanga kuwasilisha malalamiko FIFA dhidi ya Barcelona kwa sababu ya kufanya mazungumzo na mchezaji Julian Alvarez ambaye bado ana mkataba halali.

Stunning! Julian Alvarez scores twice against Atletico Madrid in the derby!  - Yahoo Sports

Siku ya jana mchezaji huyo wa Atletico aliweka wazi kuwa amezungumza na timu yake kuwa anataka kuondoka klabuni hapo ili kutimiza ndoto zake.

 

“Nataka kuwa mkweli nilizungumza na Atlético na nikawaambia wazi kwamba nina hamu ya kuondoka na kujiunga na klabu mpya hivi karibuni.”Alisema Alvarez muda mchache kabla ya timu yake kutoa taarifa kuwa mchezaji huyo hauzwi.

 

Taarifa ya Atletico imeweka wazi kuwa“Kila mtu anajua kuwa ni klabu inayocheza nje ya kanuni. Lakini safari hii wamekutana na klabu ambayo haitapuuza jambo hili kwa kucheka tu,” Atlético walisema 

 

“Tayari tumeona namna Barcelona wanavyofanya kazi. Kwa mfano, wakati Atlético walikuwa wakijiandaa kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus, Barça walikuwa wakiahidi kamisheni kwa dada yake Griezmann, familia yake, na hata mchezaji mwenyewe” Imesema taarifa ya Atletico.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet