pmbet

Atlético vs Barcelona? “Natamani wote wapoteze" - Mourinho

Eric Buyanza

November 7, 2026
Share :

Kocha mkuu wa Real Madrid, José Mourinho, ametoa kauli ya kufurahisha kuelekea mtanange mkali utakaopigwa Jumapili kati ya Atlético Madrid na Barcelona, akisema hamu yake kubwa ingekuwa ni kuona timu hizo zote mbili zikipoteza mchezo huo.

 

Mchezo huo wa raundi ya 12 ya La Liga utakaopigwa kwenye uwanja wa Metropolitano unakutanisha timu mbili za juu kwenye msimamo, huku Barcelona wakiwa kileleni kwa alama 30 na Atlético wakifuata katika nafasi ya pili kwa alama 28, wakati Real Madrid ya Mourinho ikiwa nafasi ya tatu na alama 27.

 

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa Real Madrid dhidi ya Valencia, Mourinho aliulizwa anapendelea timu gani ishinde kati ya wapinzani wake hao wakubwa wa mbio za ubingwa.

 

“Atlético dhidi ya Barcelona? Ningependa zote mbili zipoteze.Kwa bahati mbaya, hilo haliwezekani.” alisema Mourinho.


Unamuunga mkono nani siku ya Jumapili?

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet