pmbet

Atletico wasisitiza Julian Alvarez hauzwi kwenda Barcelona.

Joyce Shedrack

August 27, 2026
Share :

Klabu ya Atlético Madrid imetoa taarifa rasmi ikithibitisha kuwa wameunga mkono kwa kauli moja kuhusu uamuzi wa klabu hiyo kutokufanya au kuendelea na mazungumzo yoyote na FC Barcelona kuhusu usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Julián Álvarez.
Julian Alvarez reveals stance on Premier League return as Arsenal target  former Man City forward | FOX Sports
Atlético Madrid imesisitiza kuwa FC Barcelona haikufuata misingi ya kitaalamu na heshima inayotakiwa katika soko la usajili, na hivyo kuzuia uwezekano wowote wa mchezaji huyo kuelekea Camp Nou majira

"Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Atlético Madrid wameeleza kwa kauli moja kuunga mkono kikamilifu uamuzi wa klabu wa KUTOFANYA mazungumzo ya usajili wa Julián Álvarez kwenda Barcelona.

"Atlético ipo wazi kufanya mazungumzo ya kawaida yanayotokea katika soko la usajili, lakini siku zote kwa njia ya kimaadili, kitaalamu na kwa heshima kati ya klabu na klabu.

"Tunaunga mkono kikamilifu msimamo uliotolewa awali na klabu kuwa Barcelona HAWAKUKIDHI vigezo hivi, na kutokana na hilo, hatuna mazungumzo, wala hayatakuwepo mazungumzo yoyote nao kuhusu usajili wa Julián Álvarez.

"Atlético Madrid ina imani kuwa mchezaji wetu ataelewa uamuzi huu na ataweka umakini wake katika kufanya kazi kwa njia bora zaidi ili kuisaidia klabu kufikia malengo yake, kama alivyofanya katika misimu miwili aliyoitumikia jezi ya klabu hii."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet