Atoroka na mke wa bosi baada ya kucheleweshewa mshahara
Eric Buyanza
February 26, 2024
Share :
Kilichotokea huko Lusaka nchini Zambia, mwezi wa August mwaka 2020, hakitakuja kusahaulika kirahisi kwenye kichwa cha bosi mmoja mwenye asili ya uchina.
Bosi huyo siku zijazo huenda atafikiria mara mbili kabla ya kuchelewa kuwalipa mshahara wafanyakazi wake, hasa wanaume.
Hii ni baada ya mmoja wa wafanyakazi wake wa kiume kutoroka na mkewe baada ya yeye [bosi] kushindwa kuwalipa mshahara kwa wakati.
Baada ya muajiri huyo kumtafuta mke wake bila mafanikio ndipo kijana huyo alipoamua kumtumia ujumbe wa whatsAppp wenye picha.
Picha hiyo ilimuonyesha mama kichina (mke wa bosi) akiwa amelala kifuani kwa kijana wa kizambia, na chini yake jamaa akaandika "Sihitaji tena mshahara".