pmbet

Atumbuliwa kwa kupokea jokofu la nyumbani kwa ajili ya kuhifadhia damu

Eric Buyanza

April 13, 2024
Share :

Mkurugenzi wa Huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Rashid Mfaume, ameagiza Mfamasia wa Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kuondolewa kwenye nafasi hiyo kwa kutoa taarifa ya uongo.

Mfamasia huyo anadaiwa kutoa taarifa kinzani na uhalisia wakati wa ukaguzi wa vifaa katika kituo cha afya Mwalugulu, hivyo kusababisha kupokewa kwa vifaa tofauti na vilivyoagizwa.

Dk. Mfaume alifikia uhamuzi huo juzi baada ya kubaini ukiukwaji wa ununuzi wa vifaa yakiwamo majokofu ya kuhifadhia damu kituoni hapo wakati akikagua shughuli za uendeshaji na usimamizi wa shughuli katika kituo cha afya.

Katika ukaguzi huo, Dk. Mfaume alieleza kubaini majokofu mawili ya matumizi ya nyumbani yaliyonunuliwa katika kituo hicho kwa gharama za majokofu ya kuhifadhia damu kinyume cha taratibu za ununuzi pamoja na sheria na taratibu kiafya.

“Walipokea vifaa hivi vikiwa vimefungwa na hawakufanya ukaguzi wa aina yoyote na leo (juzi) tumekuta vimefungwa lakini mfamansia anatudanganya kuwa walivikagua. Pia majokofu haya kwa ndani yameelekeza matumizi yake kuwa ni ya matunda aina ya nyanya, karoti na parachichi na matunda mengine na si damu,” alisema. 

Pia alisema tayari wataalamu wamethibitishia kuwa hayo si majokofu ya damu na gharama zake hazizidi Sh. milioni 1.5 lakini yamenunuliwa kwa Sh. milioni 3.8 na yamepokewa na mzabuni akalipwa fedha bila kufanyika ukaguzi.

Dk.Mfaume pia alimwagiza elekeza mganga mkuu wa mkoa huo kuiandikia barua ya onyo timu ya usimamizi wa shughuli za afya ya halmashauri (CHMT) ya Msalala ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo kutokana na uzembe katika usimamizi na ufuatiliaji uliobainika.

Pia Dk. Mfaume baada ya kubaini kuwapo kwa usimamizi mdogo katika ununuzi, aliielekeza timu ya usimamizi shughuli za afya mkoa (RHMT) kufuatilia wote ambao wamenunua vifaa na vifaatiba mkoani humo na kubaini uhalali wa vifaa hivyo.

“Tukiondoka tu waingie kazini kufuatilia ushirikishwaji wa watumishi na wataalamu wakati wa kuanza na kupokelewa kwa vifaa hivyo pamoja na uwapo wa barua za kuundwa kwa kamati za mapokezi ya bidhaa pamoja na taarifa zake.
NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet