Atumia Mamilioni ili kurefusha miguu apendwe, mwisho akaachwa
Sisti Herman
November 22, 2026
Share :

Mwanamitindo kutoka Ujerumani, Theresia Fischer, amefichua kutumia zaidi ya dola 162,000 (takribani TSh milioni 432) kufanya upasuaji wa kurefusha miguu yake.
Amesema aliamua kufanya hivyo mwaka 2016 akiwa na miaka 24, baada ya kushawishiwa na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani. Katika upasuaji huo, aliweza kuongeza urefu wake kwa sentimita 14.
Safari hiyo haikuwa rahisi kwani ilimgharimu maumivu makali, maambukizi na muda mrefu wa kupona. Juni 2024, madaktari waliondoa vyuma vilivyokuwa vimewekwa kwenye miguu yake.
Fischer amesema kwa sasa hataki tena kubadilisha mwili wake ili kumfurahisha mtu mwingine, bali amejifunza kujikubali alivyo.





