pmbet

Atupwa jela maisha kwa kumbaka mwanafunzi mbele ya mdogo wake

Eric Buyanza

February 29, 2024
Share :

Mahakama ya Wilaya ya Kigoma, imemhukumu Kalebo Charles (46) ambaye ni mganga wa kienyeji kifungo cha maisha na kuchapwa viboko vitano baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la nne mbele ya mdogo wake.
 

Akisoma hukumu hiyo hakimu mwandamizi wa Mahakama hiyo, Evelyn Mushi, amesema mtuhumiwa alifanya tukio hilo mnamo mwezi Septemba 03, 2023 ambapo alimchukua mhanga pamoja na mdogo wake na kuwapeleka katika nyumba ya kulala wageni ya Sebabili iliyopo manispaa ya Kigoma ambapo alitekeleza tukio hilo.
 

Akiongea nje ya mahakama mara baada ya hukumu kutolewa wakili wa serikali, Nestory Kuyula amesema mtuhumiwa alifika nyumbani kwao na muhanga kwa ajili ya kuwasalimia kwani ni familia zinazofahamiana na ndipo alipomwambia mhanga na mdogo wake waongozane nae mahali alipofikia ili mhanga akawaone watoto wa mtuhumiwa na ndipo alipofanya tukio hilo.
 

Amesema hukumu hiyo imetolwa kwa haki na ni fundisho kwa watu wengine wanaofanya ukatili dhidi ya watoto na kuiomba jamii kutoa taarifa juu ya kila tendo linalofanywa dhidi ya watoto na watu wengine ili haki iweze kutendeka.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet