Aua watoto wake 7 kwa risasi kwenye ugomvi wa kifamilia
Eric Buyanza
April 20, 2026
Share :

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Shamar Elkins ameua watoto wake saba pamoja na mtoto mwingine ambaye si wa familia hiyo katika tukio la mauaji ya risasi yaliyotokea Shreveport katika jimbo la Louisiana nchini Marekani, huku polisi wakilielezea tukio hilo kama “mzozo wa kifamilia”.
Watoto waliouawa walikuwa na umri wa kati ya mwaka 1 hadi miaka 14, kwa mujibu na shirika la habari la CBS.
Taarifa ya polisi ilisema tukio hilo la mauaji lilianza mida ya 5 asubuhi siku ya Jumapili ambapo mshukiwa alipiga risasi watu 10 kabla ya kukimbia kwa kutumia gari lililoibiwa, Polisi walimfukuza na hatimaye kumuua.
Wanawake wawili watu wazima, wakiwemo mama wa watoto hao, wako katika hali mahututi hospitalini.
Inaripotiwa kuwa mshukiwa alimpiga risasi mwanamke mmoja barabarani kabla ya kwenda kwenye nyumba ya karibu ambako aliwaua watoto 8, “mmoja kati yao hakuwa wa kwake”, polisi walisema.
Mtoto mmoja alifanikiwa kukimbia na kwenda kwenye nyumba ya jirani na kupiga simu polisi. Pia polisi walisema mshambuliaji alifanya tukio hilo peke yake. Mtoto aliyetoroka wa tisa aliruka kutoka juu ya paa na alikimbizwa hospitalini kwa matibabu, alisema Bordelon.
Akizungumza mapema Jumapili, Meya wa Shreveport Tom Arceneaux alisema: “Hili ni tukio la kusikitisha, pengine ni tukio baya zaidi la kusikitisha ambalo tumewahi kulipata Shreveport.”
BBC





