Aucho aandaliwa mechi maalumu ya kuagwa Uganda
Sisti Herman
October 29, 2026
Share :

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Uganda (The Cranes), Paul Put, amemwita kiungo Khalid Aucho kwenye kikosi cha timu hiyo kuelekea mechi mbili za kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Botswana.
Aucho alitangaza kustaafu soka la kimataifa mapema mwezi huu, lakini kocha huyo amewashangaza mashabiki wa soka nchini Uganda kwa kutaja jina la kiungo huyo wa klabu ya Sidama Coffee ya Ethiopia kwenye kikosi chake kilichosheheni mastaa 30.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa dhamira ya kocha Paul Put ni kutaka kutumia michezo hiyo kumuaga Khalid Aucho, ambaye hadi sasa ameshaitumikia The Cranes katika michezo 77 na kufunga mabao mawili.





