Aunty Ezekiel aitwa Bodi ya Filamu.
Joyce Shedrack
July 8, 2025
Share :
Bodi ya Filamu Tanzania imetoa wito kwa msanii maarufu wa filamu nchini, Aunty Ezekiel ( @auntyezekiel ) kufika katika ofisi za bodi hiyo zilizopo Kivukoni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, msanii huyo anatakiwa kufika bila kukosa siku ya Alhamisi, Julai 10, 2025, saa nane kamili mchana.
Hata hivyo, sababu za wito huo hazijawekwa wazi katika taarifa hiyo fupi kwa vyombo vya habari. Bodi ya Filamu imekuwa ikisisitiza nidhamu na ufuatiliaji wa taratibu za kisekta kwa wasanii wote nchini.