pmbet

Auza figo asomeshe mtoto, mke aiba pesa na kutoroka na mchepuko

Eric Buyanza

February 12, 2025
Share :

Huko nchini India mwanamke mmoja anatuhumiwa kumhadaa mumewe auze figo ili wapate fedha za kumsomesha binti yao lakini baadae akaiba pesa hizo na kutokomea kusikojulikana.

 

Mwanamke huyo kutoka mji wa Bengal inadaiwa alitumia miezi kadhaa kujaribu kumshawishi mumewe kuuza figo moja ili waweze kufadhili elimu ya binti yao na pesa itakayobaki itumike kwa ajili kuandaa ndoa ya binti huyo siku za baadae.

 

Ingawa alisitasita mwanzoni, lakini mwanamume huyo baadae alijikuta ameingia kwenye mtego wa mkewe akiamini kwamba figo yake ingeboresha hali ya kifedha ya familia yake na binti yao angeweza kupata elimu bila usumbufu wowote.

 

Alitumia mwaka mzima kutafuta mteja kwa njia za panya, kwani kuuza viungo vya binadamu nchini India ni kinyume cha sheria.

Miezi mitatu iliyopita hatimaye alimpata mnunuzi na baada ya kupitia uchungu mkubwa kwenye upasuaji wa kuitoa figo hiyo alikabidhi pesa kwa mkewe (rupia milioni 1, sawa na Milioni 30 za kibongo) cha ajabu mwanamke huyo alitoroka na pesa hizo akiwa na mwanaume mwingine (mchepuko).

 

Mwanaume alifanya kila jitihada kumtafuta na alikuja kumpata kwenye mji mwingine ambapo kwanza mwanamke huyo aligoma kumfungulia mlango ili waongee na pili akamwambia mumewe yuko huru kufanya lolote analotaka na kwamba hivi karibuni alikuwa kwenye 'process' za kuomba talaka yake.

 

"Fanya unavyotaka kwanza muda wowote kuanzia sasa nitakutumia barua ya kuomba talaka yangu," aliongea mwanamke huyo asiye na huruma akimwambia mumewe.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet