Auza korodani zake ili afanye maboresho ya gari lake
Sisti Herman
February 3, 2026
Share :

Katika kisa kilichowaacha wengi na mshangao, mwanaume mmoja nchini Thailand anaripotiwa kufanya uamuzi wa kuuza korodani zake ili kupata fedha za kufanyia maboresho (modifications) ya gari lake. Mwanaume huyo alijitetea kwa uamuzi huo wa kustaajabisha akisema kuwa alihitaji kiasi kikubwa cha fedha ili kulifanyia gari lake marekebisho anayoyapenda.
Kulingana na maelezo yake, ingawa thamani ya kawaida ya soko kwa "biashara" hiyo inakadiria kufikia dola milioni 1, yeye alifanikiwa kupata dili kubwa zaidi. Alidai kuwa kutokana na kuwa na "saizi kubwa isivyo kawaida," aliweza kuuza korodani hizo kwa kiasi cha dola milioni 2.7 (takriban shilingi bilioni 7 za Kitanzania).
Simulizi hii imezua mjadala mzito na sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hatua ambazo baadhi ya watu huchukua kwa ajili ya anasa zao.





