Ayrra Starr kuonekana kwenye filamu kubwa Hollywood kwa mara ya kwanza.
Joyce Shedrack
July 29, 2026
Share :
Trela rasmi ya filamu inayosubiriwa kwa hamu, Children of Blood and Bone, iliyoongozwa na Gina Prince-Bythewood, imeachiwa rasmi.
Filamu hiyo inamshirikisha nyota wa muziki kutoka Nigeria, Ayra Starr, pamoja na mwigizaji Richard Mofe-Damijo, wakifanya mwonekano wao wa kwanza katika filamu hii iliyojaa mastaa wakubwa wa Hollywood akiwemo Viola Davis, Idris Elba, Regina King, Damson Idris, Cynthia Erivo, Thuso Mbedu, Chiwetel Ejiofor na Lashana Lynch.
Children of Blood and Bone imetokana na riwaya maarufu ya mwandishi Tomi Adeyemi, na inatarajiwa kuanza kuonyeshwa rasmi kwenye kumbi za sinema duniani mwezi Januari 2027.
Baada ya trela hiyo kutoka, mashabiki wengi wameonyesha hamu kubwa ya kuiona filamu hiyo, huku wakisubiri kuona jinsi hadithi hiyo itakavyoletwa kwenye skrini kubwa.





