Azam FC ndio wamelifanya kundi kuwa gumu -Jemedari Said
Eric Buyanza
October 29, 2026
Share :

Meneja wa zamani wa timu ya Azam FC, Jemedari Said amesema uwepo wa kikosi hicho kwenye Kundi B ndio unalifanya kundi hilo kuwa gumu na kuahidi Azam FC itapita na kusonga mbele.
Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika imepangwa jana mchana na Azam FC imeangukia kundi hilo lenye timu za AS FAR kutoka Morocco, Al Ahly Tripoli kutoka Libya na Durban City kutoka Afrika Kusini.
“Watu wanasema kundi hili ni gumu, nami nakubaliana nao kwa kuwa UWEPO WA AZAM FC unalifanya kundi kuwa GUMU kama lilivyo. Ninachokiamini ni kwamba Azam FC wanatoboa kuingia Robo Fainali wahakikishe wanapata alama 9 za nyumbani kwanza..! All the best” ameandika Jemedari.





