Azam FC watozwa faini ya Milioni 50 kisa kugomea kuvaa medali.
Joyce Shedrack
July 13, 2026
Share :
Kikao cha Kamati ya Mashindano ya TFF kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilipitia taarifa za mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB (CRDB Bank Federation Cup 2026) uliochezwa Julai 4, 2026 katika uwanja wa Gombani, Pemba na kutangaza kufanya maamuzi ya matukio ya mchezo huo.

Klabu ya Azam FC imetozwa faini ya shilingi 50,000,000 kwa kosa la kukataa kushiriki kwenye sherehe za kukabidhiwa Tuzo na Zawadi kwa washindi zilizofanyika baada ya mchezo huo wa Fainali.
Adhabu hiyo ni kwa kuzingatia kanuni ya 27:7 ya Kanuni za Ligi Kuu kuhusu Vyombo vya Maamuzi.





