Azam FC yajiweka sawa kuivaa Tripoli
Sisti Herman
November 26, 2026
Share :

Kikosi cha Azam FC kimefanya mazoezi ya kwanza kwenye uwanja wa New Amaan Complex, kisiwani Unguja, Zanzibar kuelekea mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Kundi B la michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAFCC) dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.
Azam FC iliwasili kisiwani humo jana Jumatano, Novemba 25, 2026, kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa kesho Ijumaa, Novemba 27, 2026, uwanjani hapo.
Timu nyingine zilizopangwa Kundi B ni AS FAR ya Morocco na Durban City ya Afrika Kusini.





