Azam kushusha mrithi wa Maxi
Sisti Herman
May 8, 2024
Share :
Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari za michezo hasa usajili nchini Marco Mzumbe, Klabu ya Azam FC imedhamiria kufanya Makubwa msimu ujao ikiwa mpaka sasa inaelezwa imepeleka Ofa kwa Kiungo mkabaji Charve Onoya wa Maniyema ya Congo ambaye anatajwa kua na nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi kuu ya nchini humo.
Mpaka sasa Kiungo huyo ambaye ameshinda tuzo za Mchezaji bora wa Mwezi mara 2 ameshafunga bao 5 na Assist 7 huku akiisaidia Manyema kua nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi.
Onoya alicheza kwenye eneo la kiungo na kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Maxi Mpia Nzengeli wakiwa wote kwenye kikosi cha klabu ya Maniema.
Pia kiungo huyu mwenye miaka 21 ni nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo Chini ya miaka 23 na anacheza kikosi Cha CHAN.
Mbali na taarifa hizo klabu za TP Mazembe, AS Vita na FC Lupopo zote za Congo zinatajwa kuwania saini yake lakini mwenyewe ameonesha nia ya kutoka Nje ya Congo.