pmbet

Azam na Simba kuumana leo Zanzibar

Sisti Herman

September 26, 2024
Share :

Macho na masikio ya wapenda soka leo yataelekea visiwani Zanzibar ambako Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kwa mcheo mmoja wa kibabe wa dabi ya Mzizima kati ya Azam na Simba ambao utapigwa kwenye uwanja New Amaan, Unguja.

Mbungi hiyo ni ya kisasi kwani katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Mei 24, Azam ilikubali kipigo cha mabao 3-0 mbele ya Simba kwenye uwanja wa Benjamin, Dar es Salaam.

Azam ipo nafasi 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 4 wakati Simba inashika nafasi ya 6 ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 2.

Pia "battle" nyingine itakuwa kati ya viungo washambuliaji wa kati, Jean Charles Ahoua wa Simba na Feisal Salum wa Azam ambao takwimu zao zimekaribiana sana kama ifuatavyo;

Jean Charles
- Mechi - 2
- Dakika - 147
- Asisti - 3
- Goli - 1

Feisal Salum
- Mechi 4
- Dakika 295
- Asisti 3

Je unadhani timu gani itashinda leo?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet