Azam na Simba nani kumaliza nafasi ya pili?
Sisti Herman
May 28, 2024
Share :
Ligi kuu Tanzania bara itafikia tamati leo kwa michezo ya raundi ya mwiso kuchezwa kuanzia saa 10 jioni kwenye viwanja mbalimbali huku vita kubwa ikiwa ile ya kuwania nafasi ya pili kati ya klabu za Simba na Azam.
Hizi ni takwimu za timu hizo kwenye msimamo wa ligi;
Azam
- Nafasi - 3
- Alama - 66
- Magoli ya kufunga - 61
- Magoli ya kufungwa - 21
- Tofauti ya magoli - 40
Simba
- Nafasi - 3
- Alama - 66
- Magoli ya kufunga - 57
- Magoli ya kufungwa - 25
- Tofauti ya magoli - 32
Ratiba ya mechi za leo kwa timu hizo
Azam vs Geita Gold (Ugenini)
Simba vs JKT Tanzania (Nyumbani)
Je unadhani timu gani itamaliza nafasi ya pili?