"Azam timu ambayo haina mashabiki Tanzania" - Ahmed Ally
Sisti Herman
February 8, 2024
Share :
Meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally leo wakati wa hamasa kuelekea mchezo wa wa NBC Premier Leagu dhidi ya Yanga utakaopigwa jijini Mwanza amenukuliwa na PM Sports akisema kuwa wanaenda kukutana na timu ambayo haina mashabiki Tanzania.
“Nia yetu ni kumfunga Azam FC. Tunataka uwanja wote ujae mashabiki wa Simba, tunacheza na timu ambayo haina mashabiki kabisa. Tuna mchezo mgumu lakini Simba ya sasa imeimarika sana, Azam FC wamekuja wakati mbaya.”- Ahmed Ally akiongea na wanachama wa tawi la Simba Mtakuja lilipo jijini Mwanza.
Je unakubaliana na kauli hiyo ya Ahmed Ally?