pmbet

Azam wameshinda vita, kiasi kimekuwa kigingi kwa wakubwa - Mkeyenge

Eric Buyanza

August 13, 2025
Share :

Bwana mdogo amebakia zake Azam FC, kiasi kilichowekwa mezani katika mauzo yake kilikuwa kigingi kwa wakubwa. Kiufupi ilikuwa iwe hivi na imekuwa. 

Feisal alikuwa tayari kuondoka na alishafanya hadi mazungumzo binafsi na wakubwa wa Kariakoo, lakini mwisho wa siku mlima uliokuwa mbele yao katika mkataba ulikuwa mrefu, Wakubwa pumzi ndogo. 

Wameshindwa kuupanda. Azam FC imebaki na mchezaji wao, Simba SC na Yanga SC wamebaki kutoka udenda wa matamanio.

Hatujui nini kitaenda kutokea baada ya hapa. 
Kama Feisal kuongeza mkataba mpya au kumalizia mkataba wake ulioko. Maswali ni mengi, majibu ni machache. 

Katika hili Azam FC wameshinda vita, watakuwa na mchezaji kwa msimu mwingine, hii ni rahisi kwao kumuuzia project mchezaji ili aurefushe mkataba wake.

@abdulmkeyenge1 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet