Azam wamsajili beki wa Diarra Mali
Sisti Herman
April 19, 2024
Share :
Klabu ya Azam imefikia makubaliano na akademi ya Yeleen Olympique ya Mali kwa ajili ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa nchi hiyo, Yoro Mamadou Diaby.
Mlinzi huyo wa kati ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Stade Malien de Bamako, atajiunga rasmi na Azam FC kuanzia msimu ujao wa 2024/25.
Akiwa klabuni Stade Malien de Bamako, Yoro aliisadia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho, akiifungia timu yake mabao katika mechi zote mbili za robo fainali dhidi ya Dreams FC ya Ghana.
Yoro amezichezea timu zote za vijana za taifa za Mali, kuanzia ile ya chini ya 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23.
Pia alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Mali kilichoshiriki CHAN, mwaka 2022 nchini Algeria.
Beki huyo kwa mwendelezo bora wa kiwango chake kwenye michuano ya CAF na timu za Taifa hasa za vijana anatazamiwa kuwa mchezaji muhimu siku za usoni wa timu ya Taifa ambapo ataungana na nyota kama Djigui Diarra wa Yanga na Aliou Dieng wa Al Ahly.