Azam yagawa 5G kwa wajeda
Sisti Herman
February 23, 2024
Share :
Michuano ya kombe la Shirikisho Azam (ASFC) imeendelea tena jana Februari 22, 2024 kwa mechi tano huku Azam FC na JKT Tanzania wakisimamisha minara ya 5G.
Azam FC imeibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Green Warriors huku JKT Tanzania ikiitandika TMA Stars jumla ya magoli 5-1, Azam Fc 5-0 Green Warriors.
Mabao ya Azam FC jana yalifungwa na Idd Nado 32’, Kipre Junior 33’, Paul Kyabo (og) 56’, Abdul Sopu 65' na Ayoub Lyanga 83’ akihitimisha kipigo hicho cha 5G.
Matokeo mengine ya michuano hiyo jana
JKT Tanzania 5-1 TMA Stars
Tabora United 2-0 Nyamongo Sc
Ihefu SC 2-0 Mbuni Sc
Geita Gold 2-1 Mbeya City