Azam yamruhusu Dube kujiunga na Yanga
Sisti Herman
June 28, 2024
Share :
Klabu ya Azam imethibitisha kuridhia ombi la aliyekuwa mchezaji wao Prince Dube raia wa Zimbabwe aliyeomba kuvunja mkataba wake na klabu hiyo aliyoyatoa mwezi machi 2024.
Hatua hii inafuatia kitendo cha mchezaji huyo kutimiza matakwa ya kimkataba yaliyoainishwa kwenye vipengele vinavyoruhusu upande mmoja kuvunja mkataba.
Dube ambaye inadaiwa yupo kwenye rada za wananchi, klabu ya Yanga sasa yupo huru kutambulishwa na timu yoyote kama mchezaji wao.