Azam yashusha kiungo aliyewasumbua Yanga kutoka Mali
Sisti Herman
July 16, 2024
Share :
Klabu ya Azam imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Mali, Cheickna Diakite, aliyemnunuliwa kutoka miamba ya soka ya Mali, Real Bamako.
Nyota huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 19, aliyepachikwa jina la staa wa Real Madrid "Mbappe", kutokana na kasi na uwezo wake wa kuipenya safu ya ulinzi ya timu pinzani, amesaini mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya kudumu ndani viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2027.
Diakite aliwahi kuja Tanzania msimu msimu juzi akiwa klabu ya Real Bamako iliyocheza dhidi ya Yanga ambapo alikuwa mwiba mkali kwa mabeki kiasi cha kuzivutia timu vigogo za Tanzania wakiwemo Azam walimsajili.