Azam yashusha mwingine kutoka Colombia
Sisti Herman
May 30, 2024
Share :
Klabu ya Azam imethibitisha kuwa imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji raia wa Colombia, Jhonier Blanco, kutoka klabu ya Aguilas Doradas ya mji wa Rionegro, inayoshiriki Ligi Kuu ya Colombia.
Blanco mzalizaliwa wa Oktoba 18, 2000, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vya afya, kufuatuatia makubaliano baina ya klabu yake na Azam FC.
Alianzia soka lake kwenye akademi ya Club Deportivo Estudiantil kabla ya kujiunga na timu ya ligi kuu ya Aguilas Doradas.
Akatolewa kwa mkopo kwenye klabu ya daraja la kwanza ya Fortaleza. Akiwa na klabu hiyo, akaibuka kuwa mfungaji bora akiisaidia kupanda daraja. Baada ya mkopo akarudi klabuni kwake Aguilas Doradas hadi sasa ambapo Azam FC imemnunua.