Aziz Ki aziingiza vitani timu za Waarabu na Wasauzi
Sisti Herman
May 21, 2024
Share :
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari za michezo kutoka mataifa ya kaskazini, kusini na nje ya Afrika zinaeleza kuwa nyota wa klabu ya Yanga Stephanie Aziz Ki ameziingiza vitani klabu kubwa barani Afrika kama Al Ahly ya Misri na ASFAR ya Morocco na zingine tatu kutoka Afrika kusini ambazo ni Mamelod Sundowns, Kaizer Chiefs na Orlando Pirates.
Kiwango kikubwa cha Aziz Ki kwenye hatua ya makundi na mtoano za michuano ya Afrika msimu huu kimeshawishi kwa kiasi kikubwa vilabu hivyo ambapo mpaka Yanga inatolewa kwenye robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika alikuwa;
- - Amecheza mechi 8
- - Amefunga goli 1
- - Na kutengeneza goli 2
- - Ameingia kwenye timu bora ya wiki mara 2
Huku kwenye ligi kuu Tanzania bara inayoelekea ukingoni hadi sasa akiwa;
- - Amecheza mechi 24
- - Amefunga goli 15
- - Na kutengeneza goli 8
Je unadhani Yanga wanaweza kumshawishi Aziz Ki kuongeza mkataba mpya na kuendelea kusalia Yanga dhidi ya ofa za timu za Kaskazini, Kusini na nje ya Afrika.