Aziz Ki, Feitoto vita nzito kiatu cha dhahabu
Sisti Herman
March 15, 2024
Share :
Mara baada ya jana kufunga goli moja lililowapa Yanga ushindi dhidi ya Geita Gold, Kiungo mshambuliaji wa Yanga Steaphanie Aziz Ki sasa amefikisha goli 13 na anapanda juu kuongoza orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa kufunga mabo mengi zaidi kwenye ligi kuu Tanzania bara na kumzidi kiungo wa Azam Fc Feisal Salum mwenye goli 12.
Hii ndo orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa kutupia nyavuni hadi sasa;
1. Stephanie Aziz Ki (Yanga) - 13
2. Feisal Salum (Azam) - 12
3. Waziri Junior (KMC) - 11
4. Max Nzengeli (Yanga) - 9
5. Samson Mbangula (Prison) - 8
Je unadhani nani ataibuka na tuzo ya ufungaji bora mwishoni mwa msimu?