Aziz Ki tayari kuwavaa CCFA FC Jumamosi
Eric Buyanza
October 15, 2026
Share :
Baada ya kukosekana kwenye pambano la Derby Jumamosi, kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz KI anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya CCFA FC, Jumamosi.
Aziz KI raia wa Burkinafaso aliukosa mchezo wa Simba kutokana na kutumikia kadi nyekundu aliyoipata kwenye pambano na Geita Gold.
Nyota huyo ameshiriki mazoezi ya Yanga wanaojiandaa na mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Saa 9 Alasiri.






