B19 Yawekewa dau nono wachezaji wake wakiifunga Simba.
Joyce Shedrack
March 3, 2026
Share :
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa timu ya B19, Felix Makota amesema wamewekea dau nono wachezaji wao wakiitoa Simba SC katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho la TFF.
Makota amesema wanafahamu mchezo huo ni mgumu ndio maana wamewatangazia dau wachezaji wao endapo wataibuka na ushindi katika mchezo huo.
Mchezo huo wa 32 Bora unatarajiwa kuchezwa Jumamosi katika Uwanja wa Meja Isamuhyo, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.





