Baada ya kipigo cha Prison, Benchikha asepa kwao
Sisti Herman
March 7, 2024
Share :
Meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amethibitisha kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Abdelhack Benchikha ameondoka nchini leo kurejea kwao Algeria kushiriki kozi za ukocha itakayofanyika kwa siku 5.
Ahmed amesema kuwa katika kipindi hichi ambacho Simba itamkosa Benchikha kwenye michezo miwili ya ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union na Singida FG timu itakuwa chini ya makocha wasaidizi Farid na Seleman Matola.