Baada ya kumkosa Alonso, Liverpool sasa yamuwania Ruben Amorim
Eric Buyanza
March 30, 2024
Share :
Klabu ya Liverpool wameripotiwa kuanza kumnyemelea kocha wa klabu ya Sporting Lisbon, Ruben Amorim ili kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp kukinoa kikosi cha Anfield.
Chaguo hili limekuja siku moja baada ya kumkosa Xabi Alonso ambaye ataendelea kuifundisha klabu yake ya Leverkusen.
Amorim bado yuko kwenye mkataba na wababe hao wa Ureno hadi msimu wa joto wa 2026 baada ya kusaini mkataba wa miaka 4 Novemba 2022.
Hata hivyo, mkataba wake unaripotiwa kuwa na kipengele cha (kuuvunja) kinachokadiriwa kufikia euro milioni 15 ambacho kitaanza kutumika mwishoni mwa msimu.