Baada ya kunusurika kifo, akaitwa Mjapani muoga kuliko wote!
Eric Buyanza
January 9, 2024
Share :
Masabumi Hosono ndiye raia pekee wa Japan aliyenusurika kifo katika ajali ya meli maarufu ya Titanic iliyozama tarehe 15 April mwaka 1912.
Mtumishi huyo wa umma Hosono...akiwa na miaka 42 kipindi hicho, aliporejea nchini kwake baada ya ajali, alikuwa akilaumiwa na kudharauliwa na kila Mjapani kwa kujiokoa yeye binafsi na kushindwa kuokoa wengine.
Wajapan walikuwa wakimuona Hosono kuwa ndiye Mjapani muoga zaidi kuliko wote nchini humo.
Meli kubwa ya Titanic ilizama kwenye Bahari ya Atlantic ikiwa ni siku nne baada ya kuanza safari yake kutoka Southampton nchini Uingereza kwenda New York nchini Marekani.
Na ilisababisha vifo vya watu 1,500 kati ya 2,224 waliokuwemo kwenye meli hiyo, huku mali za thamani zikiharibika.
Kuzama kwa meli hiyo kulitokana na kugonga kwenye mwamba wa barafu.